Othman Masoud Makamu wa Rais Zanzibar

ZANZIBAR: RAIS na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, amemteua Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa leo Septemba 18, na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza leo.
Aidha, Othman ataapishwa Septemba 22, saa 4:00 asubuhi Ikulu ya Zanzibar.



