Serikali yaweka mkazo mifumo Uhamiaji Mtandao

DODOMA; Serikali imesema katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, ilitoa kiasi cha Sh bilioni 69 kwa ajili ya ununuzi na ufungaji wa vifaa vya mifumo ya Uhamiaji Mtandao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametoa kauli hiyo bungeni leo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magomeni, Imamu Mtumwa Vuai aliyetaka kujua serikali imejipangaje kuimarisha uwezo wa Idara ya Uhamiaji katika matumizi ya teknolojia za kisasa za utambuzi na udhibiti wa mipaka ili kuimarisha usalama.
“Uimarishaji wa matumizi ya mifumo hii ya kiteknolojia umerahisisha sana utolewaji wa huduma za kiuhamiaji sambamba na kuimarisha usalama wa nchi hasa katika utambuzi na udhibiti wa mipaka.
“Katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali ilitoa kiasi cha fedha Shilingi bilioni 69 kwa ajili ya ununuzi na ufungaji wa vifaa vya mifumo ya Uhamiaji Mtandao, kukabarati miundombinu ya majengo ya vituo ili iweze kusimikwa mifumo hiyo.
“Kuongeza uwezo wa vifaa vya kuhifadhi data na kuendesha mifumo katika kituo Kikuu cha kuhifadhi mifumo na data zinazozalishwa (National Internet Data Center) kilichoko Dar-es-Salaam na kituo cha kujikinga na majanga (Disaster Recover site) kilichoko Mazizini Zanziba,” amesema Waziri Katambii.




https://www.facebook.com/share/r/1D6j7uLbHd/