Songwe yaongoza njia mageuzi ya kiuchumi Dira 2050

SONGWE: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Mkoa wa Songwe unapaswa kutazamwa kipekee utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 kwa kujenga uchumi unaozalisha fursa, ajira.
Akizungumza katika siku ya kwanza ya Jukwaa la Dira 2050 mkoani Songwe, Prof Mkumbo amesema lengo ni kuubadilisha mkoa kutoka kuwa wa kiutawala na kuwa mkoa wa kiuchumi, kwa kuanzia kwenye fursa, kwenda kwenye uwekezaji, uzalishaji, kuongeza thamani na hatimaye mauzo ya nje.
Akizungumza katika Jukwaa la Dira 2050 katika Mkoa wa Songwe, lililoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo, Jabiri Makame, Prof Mkumbo amesema atahakikisha anapita kila mkoa kuzileta pamoja sekta ya umma na binafsi kwa lengo la kutekelezaji wa Dira 2050.
Amesema wabebaji wakubwa wa maono katika Dira ya 2050 ni sekta binafsi, hivyo ushiriki wao kwenye jukwaa hilo umekuwa wenye tija.
Prof Mkumbo pia amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa kuandaa jukwaa la Dira 2050, sambamba na kushirikisha sekta binafsi kwenye jukwaa hilo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabari Makame amesema mkoa huo una fursa nyingi za kilimo, madini, kijografia na biashara.
Pia amehamasisha ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika kuyafikia maono ya Dira 2050.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com
This site really lives up to its name. It has been a dream experience winning and withdrawing so easily. Cheers to the team at phdreamjili2.