BancABC Tanzania yaanzisha akaunti za amana

BancABC Tanzania yaanzisha akaunti za amana

BENKI ya BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara imezindua kampeni maalumu inayolenga kuwanufaisha wateja wanaofungua akaunti za amana.

Kwenye kampeni hiyo iliyoanza jana na kuendelea mpaka Desemba 15, mwaka huu, wateja wa BancABC Tanzania watakaofungua akaunti za amana watapata riba ya hadi asilimia 11 papo hapo.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kuzindua kampeni hiyo, Ofisa Mkuu Mwendeshaji BancABC Tanzania, Joyce Malai aliwataka wateja kutumia nafasi hiyo kufaidika na kampeni.

Advertisement

Alisema BancABC ipo tayari kukubali wateja kufungua akaunti za amana kwa kipindi cha robo ya mwaka, nusu au mwaka na riba italipwa papo hapo kwa akaunti zote hizo.

Meneja wa Kitengo wa Wateja wa Rejareja na Biashara, Lillian Mwakitalima alisema kinachotakiwa kufanywa na mteja ni kufika kwenye matawi nchini kote na kufungua akaunti ya amana ya muda maalumu ambayo riba hiyo italipwa papo hapo.