MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mtwara imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 45 kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Akizungumza Disemba 6, 2023 katika kilelele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi Meneja wa TRA mkoani hapa, Elirehema Kimambo amesema makusanyo hayo ni kuanzia Julai mpaka Novemba 2023 ikiwa wamevuka lengo walilojiwekea la kukusanya Sh bilioni 27 ndani ya kipindi hicho.
Uzinduzi wa maadhimisho hayo yalifanyika Disemba 4, 2023 yaliyoambatana na usiku wa tuzo kwa walipa kodi kutoka taasisi mbalimbali zilizofanya vizuri katika ulipaji kodi mwaka huu.
Amesema mafanikio ya makusanyo makaubwa ya kodi ni matokeo ya maamuzi ya serikali ya awamu ya sita ya kuufungua mkoa huo kwa kuruhusu kufunguliwa mipaka iliyokuwa imefungwa pamoja na kuruhusu zao la korosho kusafirishwa kupitia bandari ya mtwara hasa korosho inayozalishwa Lindi, Ruvuma na Mtwara.
Naibu Kamishna wa Idara ya Kodi za Ndani, Huduma za Kiufundi wa TRA, Ted Silkuwasha amesema mamlaka imefanikiwa katika maeneo mengi ya kususanyaji wa mapato.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mamlaka ilikusanya Sh trilioni 24.11 sawa ufanisi wa asilimia 57.4.
Aidha makusanyo hayo ikiwa ni lengo la kukusanya Sh trilioni 24.
76 sawa na ongezeko la asilimia 8.
2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema kupitia kodi hizo serikali imeweza kuwekeza miradi mbalimali ya kimkakati mkoni humo ikiwemo bandari, uwanja wa ndege, barabara na mingine.
‘’Haya yote yanatokana na uzalendo mkubwa unaonyeshwa na wananchi katika ulipaji wa kodi pamoja na watendaji wa mamlaka kuanzia ngazi ya mkoa na taifa kwa ujumla’’amesema Abbas
‘’Napenda kuwashukuru na kuwapongeza sana wafanyakazi wa Tra kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kukusanya mapato yanayoenda kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya nchi, na mkoa wetu ukiwa ni sehemu ya kunufaika’’amesema Abbas