Chizenga ataka amani ya nchi itunzwe

KATIKA kipindi ambacho Tanzania inapitia changamoto za kijamii na kisiasa zinazoambatana na tofauti za mitazamo na fikra, viongozi wa dini wameendelea kusisitiza umuhimu wa kulinda amani, mshikamano na utulivu wa taifa. Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza la Ulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Hassan Chizenga, katika mahojiano maalum yaliyolenga kujadili nafasi ya dini wakati wa misukosuko ya kijamii.
Sheikh Chizenga amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na dini kuu mbili—Uislamu na Ukristo—ambazo zote zinahimiza maadili ya upendo, uvumilivu na kuheshimiana. Amesisitiza kuwa ni wajibu wa viongozi wa dini kuhakikisha misingi hiyo inalindwa ili taifa liendelee kudumisha utulivu wake wa muda mrefu.
Ameeleza kuwa kihistoria, waumini wa dini tofauti nchini wamekuwa wakiishi kwa amani na kushirikiana katika maisha ya kila siku, jambo lililoifanya Tanzania kuwa mfano wa mshikamano barani Afrika. Hata hivyo, ameonya kuwa changamoto za kisiasa, maslahi ya makundi fulani pamoja na ushawishi kutoka nje vinaweza kusababisha mpasuko wa kijamii iwapo tahadhari haitachukuliwa. “Dini zote zinahimiza amani na maelewano. Tukizishikilia vizuri misingi ya dini zetu, hatutakuwa na sababu ya kugombana au kugawanyika,” amesema Sheikh Chizenga. SOMA: Amani ya nchi yatakiwa kuendelezwa

Aidha, amesisitiza kuwa tofauti za mitazamo ni jambo la kawaida na muhimu katika maendeleo ya fikra, lakini ni lazima kuweka mipaka ili zisigeuke chanzo cha migogoro au chuki. Amehimiza jamii kujifunza kukubaliana kutokubaliana huku ikiendelea kuishi kwa kuheshimiana.
Kuhusu jukumu la viongozi wa dini katika kuponya taifa wakati wa changamoto, amesema wanapaswa kuendelea kuhubiri maadili ya ucha Mungu, kutoa elimu juu ya madhara ya vurugu, na kutoa mifano ya nchi zilizokumbwa na migogoro ili kuonesha hatari ya kupoteza amani.
Pia ameonya dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, akieleza kuwa kusambaza taarifa bila uthibitisho kunaweza kuchochea taharuki na migawanyiko. Ameongeza kuwa viongozi wa dini pamoja na wanahabari wanapaswa kuwa makini katika kuchuja taarifa na kuhakikisha wanatoa ujumbe unaojenga jamii badala ya kuigawa.
Akizungumzia juhudi za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuunda tume ya kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea kabla na baada ya uchaguzi, Sheikh Chizenga amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuleta maridhiano na kurejesha imani ya wananchi kwa taasisi za taifa.
Amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuunga mkono jitihada za maridhiano na kuliombea taifa ili liendelee kudumisha amani. Ameonya kuwa kupuuza juhudi za suluhu kunaweza kuleta madhara makubwa kwa mustakabali wa nchi. Kwa ujumla, viongozi wa dini wameendelea kusisitiza kuwa ulinzi wa amani si jukumu la serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwananchi. Wamebainisha kuwa mshikamano wa kijamii, uvumilivu wa kidini na matumizi sahihi ya uhuru wa maoni ni nguzo muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa taifa lenye utulivu na maendeleo endelevu.




I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do…. http://www.giftpay7.vip
Mbn ipo waz