Byabato: Imarisheni uhusiano wa Tanzania, Kenya

NAIROBI, Kenya: Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Stephen Byabato ametembelea ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi wa ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi.

Pamoja na mambo mengine Byabato amewataka watumishi wa ubalozi huo kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo jijini Nairobi.

Katika hatua nyingine, Waziri Byabato amekutana na kupata chakula cha jioni na Wabunge wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi katika Bunge la Afrika Mashariki.

Aidha Byabato alitumia fursa hiyo kuwaasa na kuwakumbusha Wabunge kuendelea kuiwakililisha vyema Tanzania na kusimamia maslahi na misimamo ya nchi.

Waziri Byabato yupo jijini Nairobi kushiriki Mkutano wa Tano Kikao cha Tatu cha Bunge la Afrika Mashariki linalofanyika Nairobi nchini Kenya.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button