Mambo safi ushirikiano Tanzania, Somalia

DAR ES SALAM: Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ya Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Hassan Sheikh Mohamud hapa nchini imekuja kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili na kufungua njia mpya za kushirikiana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Rais Samia amesema Tanzania na Somalia zimekuwa na ushirikiano mzuri kwa muda mrefu lakini ziara hii imekuja kuimarisha zaidi mashirikiano hayo.

“Katika Sekta ya Afya na Elimu tumewapa nafasi wakitaka mualiko muda wowote waje kujifunza tupo tayari kuwasaidia, pia tumejadili ushirikiano wa kidiplomasia ambapo tutaendelea kushirikiana, tumekuwa tukishirikiana kwa muda mrefu lakini ziara ya Rais Mohamud imekuja kuimarisha zaidi ushirikiano huo” amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema haitokuwa mara ya mwisho yeye kufika nchini kujifunza masuala mbalimbali ambayo anaamini yataisadia nchi yao huku akimkaribisha Rais Samia kutembelea Somalia.

Rais Mohamud yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia Aprili 26 – 27, 2024.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button