Tanzania, Belarus kushirikiana kibiashara

DAR ES SALAAM: Serikali ya Tanzania na Belarus zimesaini mkataba wa kuanzisha mkakati maalum utakaoratibu ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya mataifa hayo mawili, ikiwa ni hatua ya kuimarisha maendeleo ya sekta mbalimbali za uzalishaji nchini.

Akizungumza kuhusu makubaliano hayo, Waziri wa Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema Belarus ni miongoni mwa nchi zilizoendelea kwa kasi katika sekta ya kilimo, hususan katika uzalishaji wa mashine za kilimo, pamoja na maendeleo ya viwanda na elimu ya teknolojia.

Ameeleza kuwa kupitia ushirikiano huo, Tanzania itanufaika kwa kujifunza uzoefu na teknolojia kutoka Belarus katika maeneo ya kimkakati, jambo litakalosaidia kuongeza tija katika uzalishaji na kukuza uchumi wa taifa.

Aidha, Profesa Mkumbo amesema makubaliano hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu ya taifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050, kwa kuvutia wawekezaji kutoka Belarus kuja kuwekeza nchini mara moja.

Pia amebainisha kuwa ushirikiano huo utafungua fursa mpya za ajira, kuimarisha biashara ya kimataifa na kuongeza thamani ya mazao ya ndani kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi shindani na endelevu.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she kaz convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website

    HERE————— http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button