Mvua yakatisha mawasiliano Kenya, Sudan Kusini

NAIROBI, Kenya – Barabara kuu ya Kitale–Lodwar–Juba imekatika kabisa na hivyo kuathiri uchumi wa eneo hilo na kuathiri mawasiliano kati ya Kenya na Sudan Kusini.

Barabara hiyo ilikatika eneo la Lous huko Pokot Magharibi kufuatia mvua kubwa kunyesha. Ndiyo barabara kuu pekee inayounganisha Kenya na kusini mwa Sudan Kusini na imeathiri wafanyabiashara wanaofanya biashara kati ya nchi hizo mbili.

Wafanyabiashara wengi hutumia barabara hiyo kusafirisha mazao mapya, aina mbalimbali za vyakula, na vifaa vya ujenzi, miongoni mwa bidhaa nyinginezo.

Hali hiyo imekwamisha madereva wa malori na madereva wa magari ya kawaida kwa siku kadhaa sasa, huku jumuiya ya wafanyabiashara wakilalamikia hali hiyo na kuitaka serikali ya Kenya kuharakisha ukarabati.

Habari Zifananazo

Back to top button