DC aagiza ubora madarasa ya awali

GEITA; MKUU wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Grace Kingalame ameagiza maofisa elimu kata kusimamia ubora wa madarasa ya awali ili kujenga mazingira rafiki kwa watoto kujifunza.

Kingalame ametoa maagizo hayo wakati wa ziara maalumu ya kukagua miundombinu ya elimu kuelekea kuanza kwa mwaka mpya wa masomo 2026.

Amesema shule zinapaswa kuzingatia muongozo wa sera ya elimu unaoelekeza madarasa yote ya wanafunzi wa awali kuwa na miundombinu bora inayoakisi mafundisho kulingana na umri wao.

“Mahitaji ya madarasa ya awali yapo na yameainishwa, kwa mjibu wa Wizara ya Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), lazima tuandae madarasa kwa kufuata utaratibu huo,” amesema.

 

Kingalame amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kusimamia ujenzi wa miundombinu ya watoto kujifunza ikiwemo michoro na alama sahihi kwa watoto kujifunza kwa urahisi.

Amesema uwepo wa maiundombinu rafiki kwa watoto siyo tu itarahisisha ufundishaji kwa walimu bali pia itawajengea ari watoto kuanza kuipenda elimu pasipo kuwa na adha yeyote.

Ameongeza pia shule zote zinapaswa kuandaa vitendea kazi kwa watoto kujifunza stadi za kazi sambamba na kupata chakula shuleni kwa ilivyoelekezwa na serikali.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Ezekiel Ntiriyo amesema ili kukidhi mahitaji ya watoto kujifunza kila mwalimu mkuu atapaswa kuainisha mahitaji yake.

Amesema ofisi ya mkurugenzi ipo tayari kufanyia kazi upungufu wote utakayowasilishwa na walimu wakuu ili kufanikisha azma ya kuweka miundombinu rafiki kwa watoto kujifunza vizuri.

Takwimu za Ofisa Elimu Mkoa wa Geita, Anthony Mtweve zinaeleza hadi kufikia Januari 2025, Nyang’hwale imeandikisha wanafunzi wa awali 5,479 sawa na asilimia 74 ya lengo la 7,372.

Amesema kwa darasa la kwanza, halmashauri hiyo imeandikisha 6,585 sawa na asilimia 88 ya lengo la wanafunzi 7,450 na hivyo Nyang’hwale ndio kinara ya uandikishaji Mkoa wa Geita.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button