TPA yapongezwa ukuaji wa bandari na uchumi

PWANI: Serikali imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa juhudi zake za kuboresha uendeshaji wa bandari nchini, hatua inayoongeza ufanisi, uwajibikaji na ubora wa huduma huku ikichangia ukuaji wa uchumi wa taifa.

Akizungumza mkoani Pwani baada ya kutembelea Bandari ya Nyamisati, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema maboresho yaliyofanyika yameifanya sekta ya bandari kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi kwa kuongeza kasi ya kuhudumia mizigo, kupunguza muda wa meli kukaa bandarini, na kuboresha mazingira ya biashara kwa wafanyabiashara na kampuni.

“Hatua hizi zimeongeza mapato ya Serikali na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama lango muhimu la biashara na usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,” amesema Kihenzile.

Aidha, ameitaka TPA kuhakikisha miradi ya ujenzi wa bandari za Bagamoyo, Kisiju na Nyamisati inawanufaisha wananchi moja kwa moja kupitia miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR), ikiwemo huduma za kijamii na uboreshaji wa miundombinu katika maeneo yanayozunguka bandari.

Kuhusu usafiri salama majini, Naibu Waziri amesema Serikali kupitia Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) inaendelea na tafiti za kitaalamu ili kubaini mahitaji halisi na kuimarisha huduma za usafirishaji wa mizigo na abiria.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abed Gallus, amesema maboresho yanayotarajiwa ni pamoja na uboreshaji wa jengo la abiria ili kuhudumia abiria 300 kwa wakati mmoja, pamoja na ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mingine ya bandari.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button