Manunuzi mahitaji ya shule yaboresha biashara Dar

DAR ES SALAAM;- ZIKIWA zimesalia siku mbili shule kufunguliwa na muhula mpya wa masomo kuanza, baadhi ya wazazi wameendelea kufanya manunuzi ya vifaa na mahitaji ya shule huku wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo wakisema mzunguko wa biashara ni mzuri.

Uchunguzi wa HabariLEO umebaini kuwa bidhaa za shule zinazonunuliwa kwa wingi katika msimu huu ni madaftari, mabegi, viatu, vikokotoo na karatasi za kufanyia mtihani huku sababu ikitajwa kuwa ni kutoakana na kuanza kwa muhula mpya wa masomo kwa shule za msingi na sekondari kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza na wengine wanaoendelea.

Akizungumzia hali ya biashara sokoni Kariakoo, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Mfaume Mfaume alisema hali ya biashara ni nzuri licha ya kuwepo kwa mzunguko wa kawaida wa mauzo kulinganisha na mwaka jana.

Alisema kutokana na Januari kuwa na mambo mengi ikiwemo wazazi kulipa kodi ya nyumba na majengo ya biashara na kulipa ada imesababisha mauzo kutokuwa na kasi kama ilivyozoeleka.

“Biashara inakwenda vizuri japo si vizuri kama mwaka jana mzunguko ulikuwa ni mkubwa lakini kwa sasa wazazi wamekuwa na kujivuta,” alisema.

Alisema kwa upande wa bei za bidhaa ni nzuri hazijapanda sana na wafanyabiashara wengi wameweka bei nafuu na rafiki kuvutia wateja kwa sababu wengi wao wanafanya biashara za mahitaji ya shule yanayofanana.

Alisema katika msimu huu wa shule kufungu liwa wazazi wengi wamekuwa wakipanga bei za vifaa kutokana na kipato chao kuwa cha kawaida “Kwa Kariakoo namna ilivyo na biashara zilivyo ushindani unakuwa mkubwa, kwa hiyo mfanyabi ashara yeyote lazima auze bei ambayo ni nafuu kwa sababu ya ushindani,” alisema.

Nao baadhi ya wazazi walisema baadhi ya mahitaji kama mabegi na viatu vya shule vimepanda bei kulinganisha na mwaka jana kutokana na uhitaji wake hasa katika muhula mpya wa masomo.

“Bei za mabegi na viatu Kariakoo kwa sasa haishikiki kwa sababu ndiyo tunayahitaji kwa sana watoto wanapofungua shule wanataka mabegi ma pya, viatu vipya; inabidi ununue, sasa utafanyaje!” Alisema Zuhura Alex.

HabariLEO ilishuhudia msongamano mkubwa wa watu maeneo ya Kariakoo na Ilala Mchikichini wakifanya manunuzi, wengi wakinunua zaidi vifaa vya shule

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button