PPRA yawapa mafunzo wafanyabiashara Dar

DAR ES SALAAM; Wafanyabiashara wapatao 500 jijini Dar es Salaam wameshiriki mafunzo maalumu ya ununuzi wa umma yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za serikali kuwawezesha wazawa kushiriki kikamilifu katika zabuni za miradi ya umma.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Dennis Simba, amesema miradi yote ya serikali yenye thamani ya hadi Sh bilioni 50 inapaswa kutekelezwa na wazabuni wa ndani.

Amewataka wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kwa kuzingatia sheria, taratibu na viwango vilivyowekwa.

Amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wajasiriamali wa kitanzania kwa kuwapatia uelewa wa sheria, taratibu na mifumo ya ununuzi wa umma, ambapo pia washiriki wamepatiwa taarifa kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye miradi ya serikali.

Amesema kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, serikali imeweka upendeleo maalumu kwa wazabuni wa ndani.

Serikali pia imeboresha mifumo ya ununuzi wa umma ili iwe rafiki, ya uwazi na inayorahisisha ushiriki wa wazawa katika zabuni za serikali.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa PPRA Kanda ya Pwani, Kenneth Ndebuka, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa mamlaka hiyo wa kuwajengea wazawa uwezo wa kushiriki kwa ushindani wa haki katika zabuni za serikali.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata na kusema imewasaidia kuelewa kwa undani mchakato wa kushiriki zabuni za serikali kwa njia sahihi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button