Kasi ya maendeleo Zanzibar uhalisia Mapinduzi ya 1964

ZANZIBAR; LEO ni maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu yalipofanyika Januari 12, 1964 baa da ya kuondolewa utawala wa kisultani ukiongo zwa na Jamshid bin Abdullah na Abeid Amani Karume kushika usukani.

Miongoni mwa maeneo yanayoeleza kwa uwazi maana halisi ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni kasi ya maendeleo iliyofikiwa tangu Mapinduzi yafanyike mpaka sasa.

Ni wazi Zanzibar imepiga hatua kubwa katika nyanja za elimu, afya, miundombinu ikiwemo ujenzi wa hoteli, viwanja vya ndege, barabara na hivyo kukuza uchumi.

Tukizungumzia eneo moja la elimu, Mapinduzi yameleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu Zanzibar hasa mka kati wa ujenzi wa shule kwa mtindo wa ghorofa na kupun guza kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa madarasa na uendeshaji wa shule kwa mfumo wa zamu ya asubuhi na mchana.

Desemba 27, 2025 Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi akifungua Shule mpya ya Msingi ya Muungano iliyopo Kibanda Maiti, Mkoa wa Mjini Magharibi alisema serikali inalenga kuongeza bajeti ya sekta ya elimu hadi kufikia Sh trilioni moja na kuifanya sekta hiyo kuwa sekta mama ya kipaumbele kwa maendeleo ya nchi.

Kama hiyo haitoshi, Dk Mwinyi alisema kuwezesha hilo serikali imeshasaini mkataba na Benki ya CRDB wa thamani ya Sh bilioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa shule 29 za ghorofa, ambapo maandalizi ya ujenzi yameanza katika maeneo ya Fuoni Kibondeni, Jumbi na Chunga kwa Unguja, pamoja na Kiuyu Minungwini, Mchanga Mdogo na Micheweni kwa Pemba kupitia mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, Serikali ya Awamu ya Nane tayari imejenga shule 35 za ghorofa, hali iliyosaidia kupun guza msongamano wa wanafunzi darasani kwa kiasi kikubwa huku walimu wapya 1,741 wakiajiriwa mwaka 2024/2025, na tayari walimu 492 wamajiriwa mwaka 2025/2026, huku lengo likiwa ni kuajiri walimu 1,500.

Tunaipongeza serikali ya Dk Mwinyi na nyingine kabla yake ikiwemo ya kwanza chini ya Karume kwa kupambana kwa vitendo kuyaweka Mapinduzi katika uhalisia wa maisha ya wananchi.

Tunatambua bado yapo maeneo yenye changamoto ya shule, zahanati, vituo vya afya, barabara, maji na miundom binu mingine lakini hatua iliyopigwa inaonekana katika sekta zote kazi imefanyika.

Kwa mfano katika sekta ya utalii, taarifa ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar inasema Zanzibar iliweka rekodi mpya ya kupokea zaidi ya watalii 106,000 kwa Julai 2025 ikiwa ni sehemu ya watalii 478,875 walioingia kuanzia Januari mpaka Julai mwaka jana.

Hivyo tunapopongeza uimarishaji wa elimu Zanzibar hatujasahau barabara zinajengwa tena kwa viwango vya lami kama ya Kitogani-Paje ya urefu wa kilometa 13.2 iliyozindu liwa hivi karibuni na Rais mstaafu, Dk Ali Mohamed Shein. Hii ndio maana ya Mapinduzi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button