Dk Mwinyi aachia huru wafungwa 17 Mapinduzi

ZANZIBAR; LEO ni kumbukizi ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika siku kama ya leo miaka 62 iliyopita am bapo Wazanzibari waliondoa utawala wa kisultani uliokuwa ukiongozwa na Sultan Jamshid bin Abdullah na kuingia wazalendo walioongozwa na Shehe Abeid Amani Karume.

Mapinduzi hayo yalileta utu na heshima kwa watu wa Zan zibar baada ya Uingereza kutoa uhuru mwaka 1963, chini ya utawala wa Waarabu walioen deleza ubaguzi na unyanyasaj kwa wananchi wa Zanzibar.

Zanzibar imepiga hatua kubwa baada ya mapinduzi ikiwa ni pamoja na kwenye sekta za elimu, afya, miundombinu, huduma mbalimbali kama nyumba, umeme, maji, uchumi na barabara. Katika kuendeleza ma fanikio hayo, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametoa msamaha kwa wafungwa 17 katika maadhimisho hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Rapey Mohamed ilieleza kuwa msamaha huo umetolewa chini ya Kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinachompa rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa mtu aliye hukumiwa kwa kosa lolote.

“Msamaha huu ni kwa jumla ya wanafunzi (wafung wa) 17 waliokuwa wakitumikia adhabu zao katika Chuo cha Mafunzo, kati yao wafungwa 11 ni wa Unguja na sita ni kutoka Pemba,” ilieleza taarifa hiyo. Ilieleza kuwa hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyeki wa Baraza la Mapinduzi kutoa msamaha kwa baadhi ya wa fungwa wa Chuo cha Mafunzo katika maadhimisho ya kitaifa kama hayo.

Mapinduzi ya mwaka 1964, yalikuwa ya lazima ili kurejesha na kujenga heshima ya Mzanzibari, jambo ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa mpaka sasa. Kabla ya Mapinduzi, maendeleo hayakuwa ya kuri dhisha kwa sababu wakoloni walizingatia zaidi maslahi yao binafsi bila kujali utoaji wa huduma bora kwa wanan chi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button