Msigwa: Serikali haijakosa fedha kumalizia uwanja Arusha
SERIKALI imesema haijakosa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Arusha, ikisisitiza kuwa mradi huo unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai, 2026 kama ilivyopangwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa kauli hiyo kufuatia taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii zikidai kuwa Serikali imeomba msaada wa fedha kutoka China ili kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.
Msigwa amesema taarifa hizo zilimnukuu vibaya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, James Millya, na kusisitiza kuwa Serikali haijakwama kifedha katika utekelezaji wa mradi huo.
“Nimeona taarifa zilizosambaa, Naibu Waziri hakueleweka vizuri. Kwa ujumla maandalizi yetu yako vizuri na miradi yote tunayoitekeleza kwa ajili ya AFCON 2027 inaendelea vizuri, ukiwemo uwanja wa Arusha. Hatujakwama kujenga uwanja wa Arusha kwa sababu ya kukosa fedha,” amesisitiza Msigwa.
Amesema ujenzi wa uwanja huo umefikia asilimia 74, huku mkandarasi akiendelea na kazi mbalimbali ikiwemo ufungaji wa paa la uwanja ili kutoa sura halisi ya mradi huo.
Msigwa amesema mkandarasi anayejenga uwanja huo amelipwa kwa wakati na sehemu kubwa ya vifaa vya kumalizia ujenzi tayari vimeshawasili katika eneo la mradi, huku kazi ya kuvifunga ikiendelea.
Ameeleza kuwa ifikapo Julai 2026, uwanja huo pamoja na viwanja viwili vya mazoezi vinavyojengwa sambamba na mradi huo vitakuwa tayari kutumika.
Aidha, Msigwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwemo kuchangia bajeti ya Serikali inayogharamia miradi ya maendeleo na uanzishaji wa miradi mipya.
Katika hatua nyingine, amewataka Watanzania kuendelea kujiandaa na mashindano ya AFCON 2027, akibainisha kuwa mashindano hayo yatatoa fursa nyingi za kiuchumi na kijamii kwa nchi.




I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com