BUWASA yawakumbuka wenye uhitaji

BUKOBA: MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) imetoa msaada na vifaa vya shule katika kituo cha watoto wenye uhitaji cha Tumaini Children Center kilichopo mtaa wa Kyakairwabwa, kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Ofisa Uhusiano wa BUWASA, Juliethi Shangali amesema wafayakazi wanawake wa taasisi hiyo na wadau wa maji wameona ipo haja ya kuwaunga mkono watoto hao katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8.

Amesema mahitaji yaliyotolewa kwa kituo hicho ni madaftari, kalamu, vifutio rula, upande wa vyakula ,mchele ,mafuta ,unga sukari, pia sabuni juisi.
“Nimepata historia ya kituo hiki nimesikitika sana, naomba wadau na jamii hata kama sio sherehe watoto hawa wakumbukwe kwa sababu ni wadogo na wanamahitaji mengi sana lakini wengine ni wale waliotelekezwa hivyo wanahitaji faraja ya karibu kama watoto wengine,”alisema Shangali.

Mwangalizi wa kituo hicho, Sister Adventina Kyamanywa amesema kuwa kituo hicho kiko chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri KKKT Dayosisi ya Kasikasini Magharibi na kina uwezo wa kulaza watoto 60 na wa sasa wapo 55.
Ameaema kuwa watoto wengi walioko pale ni wale ambao wamekuwa wakitolewa mtaani hasa ambao hawana makazi kabisa na wamepitia vitendo vya ukatili kama ubakaji ,vipigo vikali kukosa chakula na wengine ni wale ambao wamekuwa wakitumikishwa kazi za majumbani baadhi uletwa wakiwa katika hali mbaya ya mateso ya kuunguzwa mili yao na baadhi kupata ulemavu kwa wanaowaajili.

Alisema watoto wale ambao familia zao upatikana huwa wanaunganishwa na familia zao moja kwa moja na kituo kufanya ufatiliaji wa mtoto na wale ambao hawana familia ubaki katika uangalizi na kupelekwa shule na baadhi kupelekwa katika vyuo vya ufundi stadi
Akisimulia baadhi ya mifano amesema mwaka jana walipokea watoto wawili ndugu ambao baba yao alichimba shimo na kuwazika wakiwa hai mpaka walipookelewa na mtu baki na kuwaleta katika kituo hicho na sasa wanaendelea na elimu ya awali na habari njema ni kwamba baba yao alihukimiwa kifungo cha maisha jela.

“Nawashukuru BUWASA kwa kutukimbuka naomba na wadau wengine watukumbuke na kutusaidia kama sehemu ya sadaka ili kufanya hawa watoto kutimizia ndoto zao ,kwani nao wanandoto za maisha yao ya baadaye Kyamanywa.



