Walioathirika mafuriko wapatiwa msaada wa vyakula

MANYARA: WATU zaidi ya 1,163 walioathirika na mafuriko baada ya nyumba zao kusombwa na maji katika Tarafa ya Moipo Wilaya ya Simanjiro mkoani Arusha, wamepatiwa msaada wa vyakula vya Sh milioni 20 na kampuni ya kuchimba madini ya Permanet Mineral.
Akipokea msaada huo Machi 29, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandana ameishukuru kampuni hiyo kwa kuwasaidia wananchi hao na kuziomba kampuni nyingine kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani mahitaji ni makubwa.
Lulandana amesema mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha nyumba zao kuingia maji na ekari 5,429 za mazao ya maharage na mahindi kusombwa na maji.

Alisema kati ya waathirika hao 1,163 waliotoka kata ya Endiamtu na ekari 233 za mashamba,ekari 1,570 kata ya Mirerani ni watu 409 wameathirika na ekari 249 za mashamba, kata ya Shambarai watu 461 wameathirika na mafuriko na mashamba ya ekari 1,600 na Naisinyai watu 60 wameathirika na mashamba ya ekari 2,010.
Kwa upande wake mwakilishi wa hiyo, Elisha Mnyawi amesema kwa niaba ya Mkurugenzi, God Mwanga wanatoa pole kwa wote waliopatwa na maafa hayo na kampuni itakuwa nao kwa hali na mali katika kipindi chote kwa kuwa yote ni mipango ya Mwenyezi Mungu.
Mnyawi ametaja msaada uliotolewa ni mahindi magunia 100, mafuta ya kupikia madumu 318, mashuka 100, mchele kilo 500, sabuni caton 400, mafuta ya kujipaka katoni 20 na vyandarua 100.
Mnyawi ambaye pia ni Maenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara( MAREMA) ametaja vitu vingine ni madaftari 100, kalamu 200, penseli 200, kompasi 100, malapa katoni sita na chumvi katoni sita.
Naye, Frank Oleleshwa katibu wa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, James Ole Millya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kiongozi huyo ametoa pole nyingi kwa wapiga kura wake waliopatwa na majanga ya mafuriko.
“Mbunge wetu pamoja na kuwa yupo nje ya nchi, bado anafuatilia kwa karibu mafuriko haya kwa kutoa pole kwa wana Moipo na Tarafa za Terrat, Emboreet na Msitu wa Tembo na kusema kuwa amesema akirudi atawatembelea na kuwajulia hali kwa hali na mali,” alisema Oleleshwa.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani, Hans Nkya ametoa pole kwa wote waliopatwa na maafa kutokana na mafuriko hayo na kusema kuwa serikali iko mstari wa mbele katika kuwajulia hali na mali hibyo wasiwe na wasiwasi.
Nkya ametoa ombi kwa taasisi, makampuni na watu binafsi wenye uwezo kutoa msaada kwa waathirika hao kama kampuni ya Permanent mineral Ltd ilivyofanya kwani waathirika wanahitaji sana msaada kwa sasa.
Diwani wa kata ya Mirerani Salome Mnyawi,Diwani wa kata ya Endiamtu Lucas Zacharia,Diwani wa kata ya Naisinyai Taiko Kurian na Diwani wa kata ya Shambarai Julius Lemboi mbali ya kutoa pole kwa waathirika ametoa ombi kwa serikali kuandika ombi ili bwawa la Kidawashi yanakopitia mafuriko hayo litumike kwa kilimo cha umwagiliaji na uvuvi wa kitaalamu ili kuounguza athari za mafuriko katika maeneo hayo mara kwa mara.
Mmoja kati ya waathirika wa mafuriko hayo, Asha Said ambaye ni mkazi wa kata ya Endiamtu, ameishukuru kampuni ya Permanent mineral kwa kuwakumbuka katika kipindi hiki kigumu kwani kwa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba yao kuzungukwa na maji katika kitongoji cha Tupendane.




I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. the potential with this is endless…,
This is what I do….. http://www.giftpay7.vip
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com