Exim, Toyota waungana kurahisisha umiliki wa ‘gari la ndoto’

DAR ES SALAAM: Benki ya Exim Tanzania imeingia katika ushirikiano wa kimkakati na Toyota wenye lengo la kufanya umiliki wa magari kuwa rahisi zaidi na nafuu kwa Watanzania.

Kupitia ushirikiano huu, suluhisho maalum la udhamini wa magari limeanzishwa, likiwawezesha watu binafsi na biashara kununua magari mapya na yaliyotumika kwa gharama ndogo ya awali Pamoja na muda nafuu wa marejesho unaoweza kufikia hadi miaka sita.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji Saini huo, Mkuu wa Huduma za Benki kwa Wateja Binafsi na wa Kati wa Benki ya Exim Tanzania, Andrew Lyimo, alisema ushirikiano huo unaonesha dhamira ya Benki kuendelea kutoa suluhisho bunifu na zinazomlenga mteja moja kwa moja.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button