Tandahimba wapewa nguvu majanga ya moto

MTWARA; WANANCHI wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wametakiwa kutoa mapema taarifa za majanga ya moto yanapojitokeza kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 29, 2026 na Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Tandahimba, Elizabeth Mpondele, wakati wa hafla ya jeshi hilo kupokea gari la zimamoto.

Amesema ni vyema wananchi likitokea tatizo la moto wakapiga simu haraka kwenye jeshi hilo ili waweze kupatiwa huduma kabla ya madhara hayajawa makubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Michael Mntenjele, amesema kupatikana kwa gari hilo litakalosaidia kuokoa maisha ya raia na mali zao wakati wa majanga ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button