Kiswahili chazidi kung’ara duniani

KWA muda mrefu, Kiswahili kilijulikana kama lugha ya mwambao wa Afrika Mashariki. Kilisikika katika mitaa ya Dar es Salaam, masoko ya Zanzibar, vijiji vya Pwani na maeneo mbalimbali ya Kenya, Uganda na nchi jirani. Wakati huo, haikuwa rahisi kufikiria kuwa siku moja lugha hiyo ingeweza kufundishwa katika vyuo vikuu vya Marekani, Ulaya na Asia, au kutumika katika majukwaa makubwa ya kimataifa.
Kiswahili kimevuka mipaka ya Afrika Mashariki na kuwa moja ya lugha zinazokua kwa kasi duniani. Kinasomwa katika taasisi mbalimbali za elimu, kinatumika katika tafiti za kitaaluma na kinaendelea kujijengea hadhi katika taasisi za kimataifa.
Zaidi ya kuwa chombo cha mawasiliano, Kiswahili sasa kinaibuka kuwa rasilimali muhimu ya kiuchumi inayoweza kufungua milango ya ajira, biashara na uwekezaji kwa Watanzania. Ukuaji huo wa Kiswahili umeifanya Serikali ya Tanzania kuendelea kuwekeza katika juhudi za kukitangaza zaidi duniani kupitia makongamano ya kimataifa yanayowakutanisha wadau wa lugha, elimu, biashara na utamaduni.
Akizungumza kuhusu nafasi ya Kiswahili katika maendeleo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema lugha hiyo imeendelea kuwa kiungo muhimu cha maendeleo ya jamii. “Kiswahili si tu lugha ya mawasiliano bali ni nyenzo muhimu ya diplomasia, utamaduni na mtangamano inayowaunganisha watu wetu na kuchochea maendeleo endelevu katika ukanda wetu,” amesema. Katika kuendeleza azma hiyo, Julai 4 hadi 7 mwaka huu kutafanyika Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili jijini Paris, Ufaransa.
Kongamano hilo linaandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), chini ya kaulimbiu isemayo “Kiswahili kwa Amani, Mshikamano na Diplomasia ya Uchumi Duniani.”
Kwa wengi, huenda kaulimbiu hiyo ikaonekana kuwa maneno ya kawaida ya kongamano. Hata hivyo, kwa wadau wa maendeleo inaeleza kwa ufupi nafasi ambayo Kiswahili imeanza kuichukua katika dunia ya sasa.
Mhariri Mkuu wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Richard Mtambi, anasema kongamano hilo ni mwendelezo wa juhudi za kuifanya Kiswahili kuwa nyenzo ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Anakumbusha kuwa kongamano la kwanza lilifanyika Havana, Cuba mwaka 2024 na kuvutia washiriki kutoka mataifa mbalimbali.
“Hili ni kongamano la pili baada ya lile la Cuba. Safari hii tunakwenda Paris kwa lengo la kuitangaza Kiswahili, lakini pia kuonesha fursa zilizopo Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo na biashara,” anasema. Kwa mujibu wa Mtambi, kongamano hilo litatoa nafasi kwa Tanzania kuonesha bidhaa zake, huduma zake, urithi wake wa utamaduni na vivutio vya utalii kwa wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Kwa lugha rahisi, Kiswahili kitatumika kama daraja la kuunganisha watu na kufungua milango ya biashara.Anasema kaulimbiu ya kongamano hilo imejengwa katika nguzo tatu muhimu; amani, mshikamano na diplomasia ya uchumi. “Bila amani hakuna maendeleo. Bila mshikamano hakuna mafanikio. Na bila ushirikiano wa kimataifa ni vigumu kupanua fursa za kiuchumi,” anasema.
Mtambi anaeleza kuwa diplomasia ya uchumi imekuwa nyenzo muhimu kwa mataifa kutafuta masoko mapya, kuvutia uwekezaji na kuongeza kipato cha wananchi wake.Ndiyo maana, anasema, Kiswahili kinaweza kuwa sehemu ya safari hiyo ya maendeleo. Paris imechaguliwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo kwa sababu ni makao makuu ya UNESCO, taasisi iliyochangia kwa kiasi kikubwa kukuza hadhi ya Kiswahili duniani.
Mwaka 2021, UNESCO ilitangaza Julai 7 kuwa Siku ya Kiswahili Duniani na hivyo kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya kwanza ya Kiafrika kutambuliwa kwa namna hiyo. “Hii ni heshima kubwa kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Inaonesha kuwa Kiswahili sasa kina nafasi muhimu katika jamii ya kimataifa,” anasema.
Kadri hadhi ya Kiswahili inavyoongezeka, ndivyo fursa za kiuchumi zinazohusiana na lugha hiyo zinavyozidi kuongezeka. Leo hii, wataalamu wa ukalimani na tafsiri wanahitajika katika mikutano ya kimataifa, taasisi za elimu na mashirika mbalimbali duniani. SOMA: Kiswahili hazina ya Tanzania

Walimu wa Kiswahili wanapata nafasi za kufundisha katika vyuo vikuu vya Marekani, Ulaya na Asia. Wataalamu wa maudhui ya kidijitali nao wanatumia Kiswahili kufikia hadhira kubwa zaidi kupitia mitandao ya kijamii. Mfano mzuri ni vijana wanaotengeneza maudhui ya Kiswahili katika YouTube, podcast na TikTok. Kupitia majukwaa hayo, baadhi yao wamefanikiwa kujiajiri na kujipatia kipato.
Katika sekta ya utalii, wageni wanaotembelea Tanzania huvutiwa kujifunza maneno rahisi ya Kiswahili kama “Karibu”, “Asante”, “Polepole” na “Hakuna Matata”. Maneno hayo hujenga ukaribu kati ya wageni na wenyeji na kuongeza thamani ya uzoefu wao wanapotembelea Tanzania.
Mtambi anawahimiza vijana kuacha kuiona Kiswahili kama somo la darasani pekee.”Wakati umefika kwa vijana kulitazama Kiswahili kama taaluma na nyenzo ya kujiajiri. Fursa zilizopo ni nyingi na zinaendelea kuongezeka kila siku,” anasema.Anaongeza kuwa hata watu ambao hawajasomea Kiswahili wanaweza kunufaika kupitia sanaa, filamu, muziki, maigizo na uandishi wa vitabu.
Kutokana na hali hiyo, BAKITA imeendelea kutoa mafunzo na ushauri kwa waandishi chipukizi na watu wenye vipaji mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha kazi zenye ubora na ushindani. Kadri dunia inavyozidi kuikumbatia Kiswahili, ndivyo Tanzania inavyoendelea kunufaika na lugha hiyo ambayo kwa miaka mingi imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya wananchi wake.
Leo, Kiswahili si lugha ya mawasiliano pekee. Ni daraja la tamaduni, chombo cha diplomasia, nyenzo ya elimu na hazina ya kiuchumi inayozidi kufungua milango mipya ya fursa kwa Watanzania ndani na nje ya nchi.




Kukatwa miguu (amputation) hutokea kwa sababu mbalimbali za kiafya au ajali. Hizi ndizo sababu kuu:
🦵 Sababu za kukatwa miguu
1. 🩺 Kisukari (Diabetes)
* Kisukari kikisababisha vidonda kwenye miguu visivyopona
* Maambukizi makali (infection) yanapoenea hadi tishu kufa (gangrene)
* Hii ndiyo sababu ya kawaida zaidi duniani
2. 🚑 Ajali mbaya
* Ajali za barabarani
* Ajali za kazi (viwandani, mashambani, mashine nzito)
* Mifupa kuharibika vibaya kiasi cha kushindikana kutibiwa
3. 🦠 Maambukizi makali (Infections)
* Bakteria kusababisha kuoza kwa tishu
* Mfano: necrotizing fasciitis au gangrene
* Ikiwa dawa hazifanyi kazi, kukatwa huokoa maisha
4. 🧬 Magonjwa ya mishipa ya damu
* Mishipa kuziba (peripheral artery disease)
* Damu kushindwa kufika miguuni
* Tishu kufa kutokana na ukosefu wa oksijeni
5. 🦴 Saratani ya mifupa au tishu laini
* Aina fulani za cancer huweza kuenea kwenye mguu
* Kukatwa husaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa
6. 🧊 Baridi kali au kuungua vibaya
* Frostbite (baridi kali sana) husababisha tishu kufa
* Kuungua moto (burns) kali sana pia kunaweza kuharibu mguu
7. 🪖 Majeruhi ya vita au milipuko
* Risasi, mabomu au milipuko ya migodi
* Uharibifu mkubwa usiotibika
⚠️ Hitimisho
Kukatwa mguu si tiba ya kwanza, bali ni hatua ya mwisho ya kuokoa maisha pale ambapo mguu umeharibika sana na hauwezi kuponyeka.
Kukatwa miguu (amputation) hutokea kwa sababu mbalimbali za kiafya au ajali. Hizi ndizo sababu kuu:
🦵 Sababu za kukatwa miguu
1. 🩺 Kisukari (Diabetes)
* Kisukari kikisababisha vidonda kwenye miguu visivyopona
* Maambukizi makali (infection) yanapoenea hadi tishu kufa (gangrene)
* Hii ndiyo sababu ya kawaida zaidi duniani
2. 🚑 Ajali mbaya
* Ajali za barabarani
* Ajali za kazi (viwandani, mashambani, mashine nzito)
* Mifupa kuharibika vibaya kiasi cha kushindikana kutibiwa
3. 🦠 Maambukizi makali (Infections)
* Bakteria kusababisha kuoza kwa tishu
* Mfano: necrotizing fasciitis au gangrene
* Ikiwa dawa hazifanyi kazi, kukatwa huokoa maisha
4. 🧬 Magonjwa ya mishipa ya damu
* Mishipa kuziba (peripheral artery disease)
* Damu kushindwa kufika miguuni
* Tishu kufa kutokana na ukosefu wa oksijeni
5. 🦴 Saratani ya mifupa au tishu laini
* Aina fulani za cancer huweza kuenea kwenye mguu
* Kukatwa husaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa
6. 🧊 Baridi kali au kuungua vibaya
* Frostbite (baridi kali sana) husababisha tishu kufa
* Kuungua moto (burns) kali sana pia kunaweza kuharibu mguu
7. 🪖 Majeruhi ya vita au milipuko
* Risasi, mabomu au milipuko ya migodi
* Uharibifu mkubwa usiotibika
⚠️ Hitimisho
Kukatwa mguu si tiba ya kwanza, bali ni hatua ya mwisho ya kuokoa maisha pale ambapo mguu umeharibika sana na hauwezi kuponyeka..