Serikali yasifu ujenzi wa sekondari Bahi

DODOMA: Serikali imeipongeza Benki ya NMB kwa kujenga Shule ya Sekondari ya Bweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wilayani Bahi mkoani Dodoma. Mradi uliogharimu Sh bilioni 5 na kukamilika kwa asilimia 100.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Atupele Mwambene, amesema shule hiyo imejengwa kwa kiwango cha juu na ina mabweni, vitanda, madawati pamoja na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 160. Inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 2027 baada ya usajili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi, Albina Mtumbuka, amesema halmashauri iko tayari kuipokea na kuitunza shule hiyo, huku akiwataka wazazi kutowaficha watoto wenye mahitaji maalumu.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano wa NMB, Innocent Yonazi, amesema mradi huo unalenga kupanua fursa za elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu. NMB imetoa zaidi ya Sh bilioni 24 kwa miradi ya kijamii katika miaka mitano.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button