Mbaazi zaidi ya tani 100 zauzwa Pwani

PWANI: ZAIDI ya tani 100 za mbaazi zilizokusanywa na wakulima wa Chalinze na Kibaha mkoani Pwani zimeuzwa zote katika mnada wa kwanza wa zao hilo, uliofanyika Kibaha kwenye ofisi za Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU).
Meneja wa CORECU mkoani humo, Hamis Mantawela, amesema mnada huo umehusisha mbaazi kilo 101,346, ambapo Chalinze zilikusanywa kilo 53,335 na Misugusugu, Kibaha, zilikusanywa kilo 48,011.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mnada huo, Mantawela amesema bei ya juu kwa kilo moja ya mbaazi zilizotoka Chalinze ilikuwa Sh1,300, huku za Misugusugu zikifikia Sh1,330 na bei ya chini ikiwa Sh1,300.
Amesema wakulima watalipwa fedha zao baada ya wanunuzi kuingiza malipo, akieleza kuwa utaratibu huo umekuwa ukisaidia kuhakikisha wakulima wanapata fedha zao kwa wakati.

“Tunapofanya mnada, wanunuzi ndani ya siku mbili wanaingiza fedha, hivyo na wakulima nao malipo hufanyika kwa haraka,” amesema.
Mantawela amewataka wakulima ambao bado wana mbaazi nyumbani kuzipeleka katika vituo husika ili ziingizwe kwenye minada na kuuzwa, badala ya kuendelea kuzihifadhi majumbani.
Kwa upande wake, mkulima na mjumbe wa Bodi ya AMCOS ya Maneromango, Kisarawe, Abdallah Mwengia, amewataka wakulima wenye mbaazi majumbani kuzipeleka kwenye minada ili waweze kuziuza na kunufaika na mazao yao.

Akizungumzia mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Mwengia amesema umeleta mabadiliko katika biashara ya mazao kwa kuwawezesha wakulima kunufaika zaidi na kilimo chao kupitia minada.
Amesema kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, wakulima walikuwa wakikumbana na changamoto ya kudhulumiwa na madalali, hali iliyowafanya wasinufaike ipasavyo na mazao waliyolima.
Ameongeza kuwa kupitia mfumo huo, wakulima sasa wanapata malipo kwa wakati na kwa uwazi, huku wakipata fursa ya kufahamu bei ambazo mazao yao yameuzwa katika minada.-




Wow, I love how the blog highlights the agricultural growth in Pwani! It reminds me of my family’s farm back home—harvesting is always such an exhilarating time. Have you ever tried growing anything yourself? By the way, have you heard about those run 3 ? They could be a fun way to unwind after all that hard work!