Dk Tulia aeleza mageuzi yaliyoimarisha IPU

ARUSHA: RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk Tulia Ackson, amesema mageuzi yaliyofanywa ndani ya jumuiya hiyo yamewezesha mabunge kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia bila kulazimika kuchagua jambo moja pekee.
Dk Tulia amesema hayo leo jijini Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki mkutano wa IPU, akieleza kuwa mabadiliko hayo ni miongoni mwa hatua muhimu zilizochukuliwa katika kipindi cha uongozi wake, ikiwamo kuboresha kanuni na taratibu za uendeshaji wa jumuiya hiyo ili iendane na changamoto zinazojitokeza katika dunia ya sasa.
Amesema awali kulikuwa na utaratibu ambao ulifanya baadhi ya hoja zinazohusu changamoto za kibinadamu na usalama duniani kushindanishwa, hali ambayo ingeweza kusababisha suala moja kuchaguliwa huku mengine yakikosa nafasi ya kujadiliwa.
“Hatuna haja ya kusema tujadili jambo moja halafu lingine lijae baadaye. Dunia inapitia mambo mengi kwa wakati mmoja na yote yana umuhimu wa kujadiliwa,” amesema.
Ametoa mfano wa majanga ya kibinadamu yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na migogoro katika maeneo mbalimbali duniani, akisema mfumo mpya unatoa fursa ya masuala hayo kujadiliwa kwa upana bila kuyafanya yashindane kwa kura ili kupata hoja moja ya kupewa kipaumbele.
Kwa mujibu wake, changamoto zinazotokea katika nchi mbalimbali, ikiwamo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan na maeneo ya Sahel, pamoja na migogoro mingine yenye athari za kimataifa, zinaweza kujadiliwa ndani ya jukwaa hilo kwa kuzingatia athari zake kwa binadamu na amani duniani.
Dk Tulia amesema Tanzania, kupitia nafasi yake katika uongozi wa IPU, imeendelea kushiriki katika kuimarisha diplomasia ya kibunge, huku mkutano wa IPU unaofanyika Arusha ukiwa fursa ya kuonesha uzoefu wa Tanzania katika uendeshaji wa taasisi za kidemokrasia na ushirikishwaji.
Aidha, amesema IPU imeendelea kuchukua hatua kuhakikisha makundi mbalimbali yanawakilishwa katika shughuli za mabunge, hususan wanawake na vijana, akieleza kuwa baadhi ya mabunge ambayo awali hayakuwa na wanawake yameanza kufanya mabadiliko baada ya juhudi za ushirikishwaji.
Amesema utaratibu huo una umuhimu kwa kuwa mkutano wa Arusha unatarajiwa kuwaleta pamoja zaidi ya wajumbe 2,000 kutoka mabunge ya nchi zaidi ya 180, hivyo uwakilishi huo unatakiwa kuzingatia makundi mbalimbali.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow detafils here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com