TSC: Walimu wana jukumu Dira 2050

DODOMA: TUME ya Utumishi wa Walimu (TSC) imewataka walimu wote nchini kuisoma, kuielewa na kuitekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan nguzo ya pili inayohusu uwezo wa watu na maendeleo ya jamii.

Nguzo hiyo inalenga kujenga taifa lenye watu wenye ujuzi, maarifa na uwezo wa kukabiliana na ushindani katika dunia inayobadilika kwa kasi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa TSC, Profesa Masoud Muruke, Oktoba 1, 2026 jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani yatakayofanyika Oktoba 5 mwaka huu katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Mwalimu ni Msingi wa Elimu Bora, Ujuzi na Ubunifu kwenye Njia ya Kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”

Profesa Muruke amesema maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani ni fursa muhimu ya kutambua mchango wa walimu katika jamii na maendeleo ya taifa.

Amesema wajibu wa walimu si kufundisha na kulea kizazi pekee, bali pia kuwaandaa vijana kuwa na uwezo wa kukabiliana na ushindani katika dunia inayobadilika kwa kasi.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Profesa Muruke amesema yamejikita zaidi katika kutoa elimu kwa walimu na jamii kwa ujumla kuhusu utumishi wa walimu, ili kuwawezesha walimu kufahamu misingi ya utumishi wao.

“Katika kuadhimisha Siku ya Mwalimu Duniani kwa mwaka huu tunatarajia kufanya mambo makuu mawili. Mosi, kuwakumbusha wadau juu ya siku hii muhimu, malengo yake na kile ambacho Serikali imeendelea kufanya katika kutimiza malengo ya maadhimisho haya muhimu. Pili, tumeandaa maonesho yanayofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma,” amesema.

Kuhusu miaka 10 ya TSC, Profesa Muruke amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa walimu kutokana na historia ya usimamizi wa ajira, maadili na maendeleo ya walimu, ambayo imepitia hatua mbalimbali tangu uhuru wa Tanzania Bara.

Siku ya Mwalimu Duniani huadhimishwa kila mwaka Oktoba 5 kwa lengo la kutambua na kuenzi mchango wa walimu katika kuendeleza maarifa, malezi na maadili ya vizazi vijavyo, pamoja na kuelimisha jamii kuhusu changamoto zinazowakabili walimu.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button