TCD: Mazungumzo nguzo ya demokrasia

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Dorothy Semu, amesema taasisi hiyo itaendelea kuunga mkono majukwaa yanayowezesha mazungumzo, uvumilivu, ushirikishwaji, kuheshimu tofauti za kisiasa na utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani na kisheria.
Semu amesema hayo leo, Oktoba 7, 2026, jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Uongozi Mpya na Nembo ya Baraza la Vyama vya Siasa, huku akisisitiza umuhimu wa kujenga demokrasia kupitia ushiriki wa wananchi, vyama vya siasa, Serikali, asasi za kiraia, vyombo vya habari na taasisi nyingine za kitaifa.
Amesema TCD inaamini demokrasia imara inahitaji kuwepo kwa mifumo ya kudumu ya mazungumzo kati ya wadau wa kisiasa na kijamii, badala ya mazungumzo kuibuka wakati wa migogoro pekee.
Kwa mujibu wa Semu, mazungumzo yanapaswa kuwa sehemu ya utamaduni wa kisiasa nchini ili kuwezesha wadau kujadili tofauti zao, kusikilizana na kutafuta suluhisho kwa njia ya amani na inayozingatia sheria.
Aidha, ameendelea kusema TCD itaendelea kuunga mkono juhudi zinazolenga kujenga mazingira ya kisiasa yanayoheshimu tofauti za mitazamo na kuwezesha ushiriki wa wadau mbalimbali katika masuala ya demokrasia na utawala.
“Maridhiano si kusahau tofauti, maridhiano si kuacha misimamo, wala si kushinikiza upande mmoja kukubali upande mwingine. Maridhiano ni kujenga mazingira ambayo tofauti zinaweza kujadiliwa, malalamiko yakasikilizwa, makosa yakatambuliwa na suluhisho likatafutwa bila kuvunja mshikamano wa kitaifa,” amesema Semu.



❤️ World hot and horny girls are waiting for you join here ………………..> https://da.gd/girls66