Mkutano kimataifa viwango vya nafaka, kunde waanza Dar

DAR ES SALAAM; Serikali ya Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kuimarisha matumizi ya viwango, usalama na ubora wa bidhaa za chakula, uongezaji thamani wa mazao ya kilimo na biashara ya haki kwa maendeleo endelevu ya uchumi.

Kauli hiyo imeelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Aristides Mbwasi, wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 45 wa Kamati ya Kiufundi ya Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) kuhusu nafaka na nikunde, umeanza Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2026..

Amesema Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lina jukumu muhimu la kuandaa na kupitisha viwango, kupima bidhaa na kuhamasisha uzingatiaji wa viwango, ili kuhakikisha bidhaa zinakidhi matakwa ya usalama na ubora.

Mkutano huo unatoa fursa kwa TBS na wataalamu kutoka nchi mbalimbali kubadilishana uzoefu na kuchangia uandaaji wa viwango vya kimataifa vinavyolenga kuimarisha usalama wa chakula, kulinda afya za watumiaji, kuwawezesha wazalishaji wa ndani na kuongeza ushindani wa mazao ya nafaka na mikunde katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.

Amesema kupitia ushiriki wake katika shughuli za kimataifa za uandaaji wa viwango, TBS inaendelea kuunga mkono ajenda ya serikali ya kukuza viwanda, kuimarisha ubora na usalama wa bidhaa pamoja na kuwezesha biashara ya haki kwa maendeleo endelevu ya uchumi wa Tanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button