Vyuo vyatakiwa kuweka mkazo mafunzo kwa vitendo

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, amesema mafunzo kwa vitendo bado hayajapewa kipaumbele cha kutosha katika vyuo mbalimbali nchini na kusababisha wahitimu kutojua mahitaji ya soko, jamii na kiuchumi.

Kutokana na hali hiyo amevitaka  vyuo mbalimbali nchini, vihuishe mitaala yao, ili kukabiliana na changamoto za ajira ikiwemo mitaala ya biashara na uongozi.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Othuman Mtuka kwa niaba ya Dk Nchemba kwenye Mahafali ya 24 ya Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA) jijini Arusha.

Amesema wahitimu hao anaamini watatatua changamoto za jamii, ikiwemo kujua mahitaji ya soko kwa jamii.

Ametoa rai kwa vyuo mbalimbali haswa katika fani za uhasibu, fedha na biashara kuhakikisha wanatumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama),  ili kuendana na kasi ya teknolojia.

Mmoja kati ya wahitimu hao ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwalla ameomba wahitimu wenzake kutumia Tehama, ili kwenda na wakati, ikiwemo kusimamia vyema miradi ya maendeleo, kwani elimu inayotolewa na IAA inamfanya mwanafunzi kujikwamua kiuchumi.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button