Madaktari bingwa na bobezi kutibu bure Pwani

PWANI; Madaktari bingwa na bobezi wanatarajia kuweka kambi ya matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, ambapo huduma hizo zitatolewa bure.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kunufaika na kambi kuanzia Novemba 16 hadi 20, 2026.

Nyongo amesema kuwa kambi hiyo itatoa huduma za uchunguzi, ushauri, matibabu na upasuaji katika maeneo mbalimbali, ikiwemo magonjwa ya moyo, macho, figo, kisukari, saratani, mifupa, afya ya akili, watoto na magonjwa mengine.

“Baadhi ya huduma zitatolewa bila malipo, ikiwemo upimaji wa sukari, uchunguzi wa homa ya ini na upasuaji wa mtoto wa jicho pia bima zote za afya zitakubaliwa, huku huduma nyingine zikitolewa kwa gharama nafuu zilizowekwa na Serikali,”amesema Nyongo.

Kambi hiyo itahusisha madaktari bingwa na wabobezi kutoka mikoa ya Iringa, Singida, Morogoro, Pwani na Dodoma, pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button