Serikali yaendelea kuimarisha mapato bahati nasibu

DAR ES SALAAM: FAIDA kwa serikali na jamii kupitia shughuli za michezo ya kubahatisha zimeelezwa kuwa sehemu muhimu ya mchango unaotarajiwa kutoka kwa kampuni zinazojihusisha na sekta hiyo, huku kampuni mpya ya BetSasa ikitakiwa kuzingatia maadili na ustawi wa vijana.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe, wakati wa uzinduzi wa kampuni ya BetSasa jijini Dar es Salaam.

Mbalwe alisema kampuni zinazofanya shughuli hizo zinapaswa kuhakikisha zinarejesha kwa jamii kwa kusaidia sekta za afya, elimu, michezo na maeneo mengine muhimu ya maendeleo.

“Tunawakaribisha BetSasa katika soko la Tanzania. Tumeona wameanza vizuri kwa kuja na kampeni hii inayolenga kuwazawadia wateja wao zawadi zenye thamani kubwa ikiwemo gari jipya la kisasa.

“Hata hivyo, tunatoa wito kwao na kampuni nyingine katika sekta hii kuongeza tija ya shughuli zao kwa kuhakikisha wanarejesha kwa jamii kusaidia sekta za afya, elimu, michezo na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,” alisema.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa BetSasa, Jimmy Kenneth, alisema kampuni hiyo imezindua kampeni ya mwaka mmoja iitwayo Kusanya Point Usepe na Jetour, inayohusisha zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu.

Alisema kila wiki wateja watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, huku kila baada ya miezi mitatu mshindi mmoja akijinyakulia gari jipya aina ya Jetour.

Kenneth alisema kampuni hiyo imejipanga kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria, kanuni, masharti, taratibu na miongozo ya mamlaka zinazosimamia michezo ya kubahatisha, pamoja na kutekeleza wajibu wake kwa jamii.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button