Wakulima walipwa Tril 2.9 mazao ya kimkakati

TUME ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imesema tani trillioni 1.009 za mazao ya kimkakati ya tumbaku, kakao, pamba , chai , ooya , choroko , korosho , kahawa, mkonge na dengu yaliunzwa kupitia vyama Vya ushirika ,ambapo jumla ya Sh trillioni 2.9 zililipwa kwa wakulima kati ya mwaka 2021/2022 hadi 2022/2023.
 
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika , Dk Benson Ndiege amesema hayo Mei 17, 2023 mjini Morogoro kwenye taarifa yake kabla ya Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Dk Mussa Ali Mussa kufungua mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika katika Kanda ya Mashariki kwa maofisa 78 wa ushirika wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
 
Dk Ndiege ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa TCDC amesema , Tume hiyo hadi sasa inasimamia Vyama vya Ushirika 7,300 vyenye wanachama takribani milioni 12 katika sekta mbalimbali ikiwemo , kilimo, mifugo , uvuvi , madini, nyumba , fedha , biashara ndogo na nyinginezo.
 
Mrajis wa vyama vya ushirika nchini amesema licha ya mauzo ya tani hizo na kiwango hicho cha fedha kilicholipwa kwa wakulima , kwa mwaka 2021/2022 serikali kupitia Mamkala za Serikali za Mitaa ilipokea jumla ya Sh bilioni 15. 144 zikiwa ni fedha za ushuru utokanao na zao la korosho pekee, kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.

“ Bila kuwa na mfumo wa Ushirika hizi takwimu tusigeweza kuzipata na tusingejua ni namna gani mazao na shughuli nyinginz zinazvyochangia pato la serikali na hizi bilioni 15 karibu bilioni moja zikikuwa ni mikoa miwili tu mkoa wa Mtwara na Lindi kwenye zao moja tu la Korosho” amesema Dk Ndiege

Dk Ndiege licha ya fedha za ushuru kwa zao hilo, kiasi kingine cha sh bilioni 1. 041 zilipokelewa kama ushuru kutoka katika zao la Kahawa kwa mkoa wa Kagera pekee.

Kuhusu upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo , Dk Ndiege amesema katika mwaka 2021/2022 , pembejeo za kilimo zenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 397.7 zilinunuliwa kupitia mfumo wa Ushirika .

Dk Ndiege amesema ,uratibu wa masoko ya mazao mengine yasiyo ya kimkakati na kuwezesha serikali kuongeza mapato yake kupitia ushirika ambapo mwaka 2021/2022 kilo 79,170,426 za zao la ufuta zenye thamani ya Sh bilioni 245 .1 zilipatikana .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button