Mkurugenzi Liverpool kuanza na Mac Allister

LIVERPOOL imekamilisha usajili wa mkurugenzi wa michezo, Jorg Schmadtke na baada ya kusaini mkataba, ameingilia kati usajili wa kiungo, Mac Allister kutoka Brighton & Hove Albion.

Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo wa zamani kutoka Sky Sport, Fabrizio Romano imeeleza kuwa Schmadtke pia ataanza kushughulikia suala la Fabio Carvallo ambaye ameripotiwa kutaka kuondoka klabuni hapo.

Mike Gordon, Rais Fenway Sports Group, mmiliki  wa Liverpool amesema: ” Jorg atafanya kazi na idara zingine za timu yetu katika kutoa ushirikiano kwa Jurgen Klopp.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button