Rais Samia: Msiogope kushirikiana na wakosoaji

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka viongoziĀ  mbalimbali kushirikiana na wadau wanaohisi wana mchango mzuri kwenye maendeleo ya taasisi zao.

Rais Samia amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kuangalia kwenye kona mbalimbali, ili kupata usaidizi kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa maendeleo ya taifa.

“Mkisoma kwenye mitandao huko tunakosolewa sana kulia, kushoto Kaskazini, Kusini mpaka nje, sasa wale mnaohisi wana mchango mnaweza kushirikiana nao wakafikiri na sisi ili tukaondosha lile vuguvugu la kwamba wamefikiri nini au wamefanya nini”

“Kila mnayemuona anafaa leteni listi yao tuwafanyie vetingĀ  tushirikiane nao,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ametoa wito huo leo Julai 14 Ikulu Dar es Salaam, wakati wa uapisho wa viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button