TPDC yaja kivingine upatikanaji gesi

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC), Mussa Mohamed Makame amesema shirika hilo lipo kwenye mchakato wa kutengeneza kituo mama cha gesi Dar es Salaam, ili kurahisisha upatikanaji wa gesi nchi nzima.

Akizungumza leo Julai 20,2023 jijini Dar es Salaam Makame amesema shirika hilo limedhamiria kutoa huduma ya gesi nyumbani na kwenye magari, hivyo ni lazima wawe na vituo kwa ajili ya huduma hizo.

” Mradi tunaotekeleza sasa ni kujenga kituo mama cha usambazaji wa gesi iliyoshindiliwa, tunajenga maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam, kituo hicho kitakuwa kinashindilia gesi ili itiwe kwenye malori ambayo yatakuwa yakisambaza gesi katika vituo dada vitakavyojengwa, lakini pia kitakuwa kinajaza magari palepale,” amesema Makame.

Mkurugenzi huyo amesema wametoa pia fursa kwa kampuni binafsi kujenga vituo vitakavyotoa huduma ya gesi, ili kufikia lengo la kusambaza huduma hiyo maeneo mbalimbali Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafutaji na uendelezaji gesi asilia, Keneth Mutaonga amesema shirika hilo lipo katika hatua za mwisho kuelekea kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa gesi ambao utaongeza gesi , pato la taifa na kutengeza ajira.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile amesema miradi hiyo ina faida kubwa kwa taifa na kuwataka waandishi wa habari kuisemea miradi hiyo pamoja na kutoa uelewa kwa wananchi, ili kuondoa baadhi ya upotoshaji ambao umekuwa ukisambazwa kwenye jamii juu ya masuala mbalimbali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button