NHC kutoa ekari 12 uwanja wa michezo Kawe

EKARI zaidi ya 12 zitakabidhiwa na Shirika la Nyumba la Taifa la (NHC) kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo Kawe jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah amesema hayo Dar es Salaam leo, wakati akizungumza na wahariri jijini Dar es Salaam.
“Kwa bahati nzuri kwa watu wa michezo kutakuwa na Sports Arena pale, ambazo serikali inajenga, tutawakabidhi ardhi ekari karibu 12 kwa ajili ya kujenga Mordern sports Arena.
“Michezo yote ya ndani na matamasha makubwa yatakuwa yanafanyikia pale Kawe Tanganyika,” amesema.
–



