Baleke, Miquissone Onana hatihati leo

SIMBA SC mpaka sasa haijawasilisha vibali vya wachezaji wa kigeni, kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka (TFF) iliyotolewa leo.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano, TFF imesema Singida FG pia haijafanya hivyo.
TFF imezikumbusha klabu hizo kuwa wachezaji ambao hawajapata vibali hivyo hawataruhusiwa kucheza mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii.



