Washauri mwongozo mazingira mazuri ya biashara

SERIKALI imeshauriwa kupeleka bungeni muongozo wa kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini blueprint Ili kuwa ni wa kisheria na kuweza kutekeleza yale yaliyokusudiwa.
Aidha imeshauriwa kuhakikisha uwepo wa umeme wa uhakika utakaochangia wenye viwanda kuimarisha uzalishaji na kuendelea kukuza biashara nchini na nje ya nchi.
Ushauri huo umetolewa Leo Dar es Salaam katika maonesho ya kimataifa ya viwanda (TIMEXPO) wakati wadau wakijadili mada iliyohusu fursa changamoto na suluhisho.
Kuhusu blueprint, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Ulega Mussa amesema iwapo nchi inataka kuendeleza sekta ya viwanda,uzalishaji na hata biashara kuweza kufika nje ya nchi ipo haja kuweka mazingira mazuri ya uzalishaji.
Amesema mwekezaji yoyote anahitaji kuona mazingira mazuri na ndio maana mkakati wa serikali wa bluuprint uliokusudia kutekeleza hayo.
Amesema makusudi hayakutimia kutokana na kutokuwa ni wa kisheria,hivyo unahitaji kupelekwa bungeni ili malengo ya uandaaji wake yaweze kutimia na sekta ya viwanda iongeze uzalishaji.
” Blueprint ilitakiwa kuwa na ratiba ndani yake kwamba kuna baadhi ya taasisi zilitakiwa ziondoke au nyingine zitengenezwe lakini Kwa kuwa haikopo kisheria halitekelezeki,” amesema na kuongeza kuwa lengo la bluuprint kuhakikisha ubora wa mazingira yaweze ya kuvutia na kuwa na uwekezaji mkubwa wenye viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa zitakazouzwa kwa wingi na wazalishaji kuwa na ushindani.
Almesema jambo lingine la kuangaliwa katika kukuza viwanda ni kuhakikisha vinasomana na sekta nyingine na visiwe vyenyewe na kulitaka shirikisho la wenye viwanda CTI kuhakikisha wanakuwa na mkakati wa kuwezesha hilo.
Ulega amesema viwanda na biashara ndio injini ya kukua kwa uchumi nchini na kwamba takwimu zinaonesha kuwa Tanzania iunafanya vizuri kwenye eneo la kuyafikia masomo ya nje.
Hata hivyo amesema sekta binafsi hawajatimia nguvu waliyo nayo ipasavyo kuhakikisha masoko mengio zaidi yanafikiwa.
Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa CTI Dk Samwel Nyantahe amesema wenye viwanda wanajadiolii namna Taifa lionaweza kuwa na umeme wa uhakika,ili kuepuka kutoathiri uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Kadhalika amesema suala la blueprint loinahitaji kutengenezwa kama iliovyokusudiwa iwe na nguvu kisheria isaidie kuongeza uzalishaji.



