Wafanyabiashara Kagera wafundwa ulipaji kodi

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amewataka wafanyabiashara kuwajibika kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanya mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo makubwa zaidi mkoani Kagera.

Akizungumza katika ufunguzi wa kampeni ya Tuwajibike inayoendeshwa na mamlaka hiyo, yenye lengo kukuza maendeleo haraka kupitia kodi, RC Mwassa alisema wafanyabiashara wanapaswa kutumia mashine ya risiti za kielekroniki pale mteja anaponunu bidhaa madukani.

Aidha RC Mwassa alisema angependa takwimu za wafanyabiashara wanaotumia mashine za EFD,s ziongezeke zaidi hivyo ametoa wito kwa TRA mkoani Kagera kuhakikisha wanapita katika maduka ya wafanyabiashara wakubwa na wafanyabiashara wa kati kuhakikisha wanakuwa na mashine hizo.

Alisema Mkoa wa Kagera unapoteza mapato mengi kwa sababu biashara nyingi zinazofanyika hazijarasimishwa hivyo wafanyabiashara wengi wanapanga bidhaaa bila kujali wingi wa mitaji yao kuliko walioko madukani hivyo TRA inapata ugumu wa kukusanya kodi.

Alisema Serikali ya Kagera itafanya kila jitihada kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kufanyia biashara ili mapato yapatikane na kila mmoja anufaike kupitia kodi yake

“Piteni mlango kwa mlango mkihamasisha matumizi ya mashine za EFD,s kinachosikitisha zaidi ni kuwa wafanyabiasha wengi wanapanga chini kwa kisingizio cha mitaji na hivyo tunapoteza mapato ,tunawaandalia mazingira mazuri mfanye biashara lakini na kodi zetu mtulipe.”alisema Mwassa.

Meneja wa TRA mkoani Kagera, Ayub Mwita  alisema kuwa Mkoa wa Kagera unawafanya biashara 23,450 kati ya hao wanaotumia mashine za kutolea Risti EFD,s  wanafikia 4,261 huku baada ya kuzindua kampeini ya Tuwajibike wanatarajia kupata ogezeko la  wafanyabiashara wapya wa kutumia mashine wapatao  1,200 kwa mwaka 2023/2024 .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button