Serikali: Tutatengeneza ajira milioni 7

DAR ES SALAAM: Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kutengeneza nafasi za kazi zaidi ya milioni 7 ifikapo 2025, ikisisitiza umuhimu wa maendeleo endelevu ya kiteknolojia ili kuongeza tija.
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango ameuambia mkutano wa 7 wa Washirika wa Kijamii Afrika unaofanyika jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kuwa serikali imeweka kando mikakati kadhaa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uchumi unatengemaa ili kufikia lengo la kitaifa.
Mkutano huo ulioandaliwa na ATE na IOE, unaleta pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali ili kujadili na kushughulikia maendeleo na changamoto katika kubuni nafasi za ajira kwa bara la Afrika.
Zaidi ya nchi 50 zinashiriki katika jukwaa hili muhimu la mazungumzo na ushirikiano kuhusu masuala ya kazi na ajira.
Dk Mpango amesema Tanzania inajizatiti kujenga uwezo wake wa kustahimili uchumi ili kusaidia sekta binafsi kukabiliana na changamoto kama ile ya COVID-19.
“Tumeagiza kila wilaya kuanzisha kanda maalum za kiuchumi ili kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Kutoa mafunzo na kuunganisha vijana na taasisi zinazotoa mikopo nafuu,” alisema.
Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, Tanzania imetenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kutoka kila halmashauri kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Mikakati hiyo inazaa matunda, alisema.



