Muhimbili kujengwa upya

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Mkurugenzi wake Prof. Mohammed Janabi  inakusudia kuijenga upya hospitali hiyo ambapo upembuzi yakinifu umeshaanza kufanyika.

Uongozi huo leo Februari 16, 2024 umekutana na  timu inayofanya upembuzi na ushauri elekezi wa ujenzi wa hospitali hiyo Korea University Medicine Research and Business Foundation Consortium and JUNGLIM Architecture & Hyundai Asan .

Timu hiyo ilianza kazi Desemba 2023 na inategemea kukamilisha kazi hiyo Oktoba, 2024. Mradi huo utajengwa kwa awamu kadhaa na kugharimu takribani Sh bilioni 700.

Habari Zifananazo

Back to top button