Yatima washiriki chakula cha pamoja Dar

DAR ES SALAAM: WATOTO walioko katika vituo vya watoto yatima mkoani Dar es Salaam, wameshiriki chakula cha pamoja na mwanzilishi wa Taasisi ya Adonai El Roi, Ngole Ngilorit pamoja na wadau wengine.

Pamoja na kushiriki chakula hicho, watoto hao pia wameshiriki michezo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupatiwa zawadi mbalimbali yakiwemo mabegi ya shule, peni, penseli na daftari.

Mwanzilishi wa taasisi hiyo amesema jambo hilo limefanyika ili kutoa furaha kwa watoto hao wanaolelewa katika vituo mbalimbali mkoani Dar es Salaam.

Amesema taasisi hiyo imejikita kuwakomboa watoto walioko katika vituo vya watoto yatima, kwa kuwapa mafunzo mbalimbali ikiwemo biashara pamoja na ufundi, ili watoto hao waweze kusimama wenyewe katika jamii.

Amesema katika kutoa furaha kwa watoto hao wameweza kushirikiana na hoteli ya Johari Rotana pamoja na benki ya ABSA.

Akishukuru kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Restituta Richard amesema anafurahi kuona kuwa taasisi zinashikamana ili kuhakikisha wanapata elimu inayokamilisha ndoto zao.

Habari Zifananazo

Back to top button