JK asifu mafanikio SGR

MOROGORO: RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR).
Kikwete ametoa pongezi hizo Morogoro baada ya kuwasili kwa usafiri wa treni hiyo katika kituo cha stesheni ya SGR Kihonda akitoka Dar es Salaam.
Katika safari hiyo kiongozi huyo alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.
SOMA: A-Z SAFARI YA TRENI DAR- DOM
“Nimefurahi sana kupanda treni hii mpya, raha mstarehe, niliamua makusudi kupanda treni kwa maana ya kuona hatua gani tumefikia …nilipita wakati ule wa matengenezo bado wakati wa ujenzi tulifika mpaka Kilosa kwenda kuona hatua iliyokuwepo na sasa imekamilika mpaka hapa,” alisema Kikwete.
Ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa mafanikio kwenye mradi wa SGR ikiwa ni pamoja na kuanza safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro na leo zinaanza safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
“Kesho (leo) ndiyo wanaanza safari ya Dodoma rasmi hivyo hivyo polepole, ndiyo kwenda hatua kwa hatua ujenzi wa mradi huu wa SGR,” alisema Kikwete.
Amesema reli na treni za SGR vina faida kubwa kwa kuwa unatumia muda mfupi hivyo kuharakisha huduma za kijamii na kiuchumi.
“Leo (jana) tumetumia mwendo wa saa 1:49 kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro na ningekuja kwa gari muda kama huu uliotumika ningekuwa nakaribia Chalinze…unaona faida yake ni kutumia muda mfupi, unaweza kuja Morogoro ukafanya shughuli zako ukamaliza na ukapanda ten treni kurudi Dar es Salaam,” alisema Kikwete.
SOMA: https://www.trc.co.tz/pages/about-sgr
Aliongeza: “Unaweza kulala Morogoro ukafanya kazi Dar es Salaam na ukarudi Morogoro na katika mazingira ya kawaida kwa usafiri wa gari hili lisingewezekana kufanyika”.
Kikwete alisema kwa sasa treni za mizigo za SGR zina uwezo wa kufunga mabehewa mengi hivyo kusafirisha mzigo mkubwa zaidi na akasema ina manufaa kiuchumi na akatoa mfano wa muda wa kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
“Nimeambiwa hapa ukitoka Dar es Salaam saa 12 asubuhi unafika Mwanza saa nane mchana upo Mwanza unakula sangara, unatumia muda mfupi kwenye shughuli zako na siku ya pili unarudi Dar eas Salaam…ina manufaa kwa watu kusafiri kwa kutumia muda mfupi na pia inaharakisha ukuaji wa uchumi katika Taifa letu,” alisema Kikwete.
Alimpongeza Rais Samia, serikali yake, watekelezaji wote wakiwemo TRC kwa jitihada walizozifanya hadi walipofikia ukamilishaji wa ujenzi wa reli hiyo hadi kufikia Dodoma.
Kikwete aliishauri TRC ione umuhimu wa kuweka stesheni eneo la Magindo au Kwala. “Namie ninavyotokea Msoga kuja Morogoro itanichukua nusu saa kufika, ninachokiomba kwa TRC muweke kituo pale Magindo au Kwala nikishuka Kwala nachukua gari kwenda Msoga na nikitoka Msoga napanda treni,” alisema.
Kikwete alitoa mwito kwa wananchi na uongozi wa TRC waitunze reli ya SGR na treni yake ili idumu miaka mingi zaidi. “Isije kuwa baada ya miezi sita ukiingia kwenye mabehewa kumejaa mchanga, viti watu wamevichana kwa visu na tukifikia hapo sasa huo ni uharibifu…kazi kubwa ni utunzaji wa miun dombinu ya SGR,” alisema.