Wajitokeza kushiriki maonesho wajasiriamali wanawake

ZAIDI ya washiriki 100 kutoa mikoa ya Tanga ,Pwani na Dar es Salaam wamejitokeza kushiriki maonesho ya saba ya biashara ya wanawake wajasiriamali Tanga maarufu Tanga Women Gala

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii, mwanzilishi wa maonesho hayo, Latifa Shehoza amesema maonesho hayo ambayo yanaanza September 11 hadi 15 mwaka huu yanatoa fursa ya wanawake kuonesha bidhaa zao na fursa za masoko.

SOMA: Matukio mbalimbali maonesho ya Sabasaba

Amesema maonesho hayo ni sehemu ya jukwaa la kuwakutanisha wajasiriamali wanawake kwa ajili ya kujengeana uwezo lakini na kuona namna ya kulifikia soko la bidhaa zao .

“Lengo ni kuhakikisha tunawasaidia wanawake waweze kushiriki kwenye kuimarisha uchumi wa familia sambamba na kuondokana na utegemezi “amesema Shehoza.

Naye mratibu wa maonesho hayo, Nassor Makau amesema kuwa maonyesho hayo yataweza kusindikizwa na burudani mbalimbali ikiwemo elimu za biashara,utanzaji wa fedha sambamba na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Tanga

Habari Zifananazo

Back to top button