Asali kukuza uchumi wa Tanzania, China

DAR ES SALAAM :Waziri wa Viwanda na Biashara, Seleman Jafo amesema soko la asali ya Tanzania nchini China linaenda kukuza uchumi wa nchi na kuwa na tija pamoja na mashirikiano ya nchi hizo mbili baina ya China na Tanzania.
Hayo ameyasema jijini Dar es salaam kwenye sherehe ya kuaga kundi la kwanza la asali ya Tanzania kabla ya kusafirishwa kwenda China.
Jafo amesema Wananchi watanufaika na fursa ya uzalishaji wa asali ambapo soko la uhakika linaenda kupatikana hivyo inapanua nyanja mbalimbali za kiuchumi .
Aidha Jafo amesema hiyo ni kontena ya kwanda ya asali inayokwenda nje yenye tani kumi za asali zinazosafirishwa kwenda China kwa ajali ya kuuzwa hivyo kwa wananchi wanaojishughulisha na asali wataenda kupata soko la uhakika nchini China.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania MingJian Chen amesema ushirikiano baina ya nchi hizo mbili zinaenda kukuza uchumi na mashirikiano bora katika biashara na ni muhimu kwa maendeleo ya pande zote mbili .
Kwa upande wake mwakilishi wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS) Karim Solyambingu amesema wamekuwa na mashirikiano na taasisi mbalimbali hapa nchini za kukusanya sampuli za asali kila mwaka na kuzipeleka kwenye maaabara kubwa iliyopo nchini Ujerumani kwa ajili ya vipimo yenye lengo la kuhakikisha asali ya nchini ina uwezo wa kufikia masoko ya Kimataifa ikiwemo soko la Ulaya na sasa nchi imeweza kupata soko la China.
Mkurugenzi wa Kampuni ya East Africa Commercial Logistic Center Cathy Wang na Muuzaji wa asali nchini Tanzania Jackson Mponela wamesema kwao ni fursa ya kimasoko ya nje kwani sekta ya nyuki bado imelala hivyo kutatanua wigo mpana na uwanda wa mashitikiano kiuchumi .



