Maziwa Dar kushuka hadi Sh 1,500

BODI ya Maziwa Tanzania (TDB) Kanda ya Dar es Salaam imesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam bei ya maziwa itaanza kushuka katika kipindi cha masika.
Kipindi cha masika ni miezi ambayo kunakuwepo na mvua nyingi ambapo huanzia Machi hadi Julai na wakati huo kunakuwa na maji na malisho mengi kwa ajili ya mifugo, ikilinganishwa na Julai hadi Februari ambao ni msimu wa kiangazi.
Mteknolojia wa Chakula kutoka Bodi ya Maziwa Kanda ya Dar es Salaam, Francisco Juma ameiambia HabariLEO kuwa uzalishaji wa maziwa unatofau tiana kulingana na msimu.
“Uzalishaji unatofautina kulingana na msimu, kipindi cha masika uzalishaji unaongezeka kutokana na kuongeka kwa maji na malisho,” alisema.
Aliongeza kuwa kwa sasa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ng’ombe hawapati virutubisho vya uzalishaji wa maziwa kwa wingi.
Juma alisema Mkoa wa Dar es Salaam si wazalishaji wakuu wa maziwa bali wa nategemea zaidi maziwa kutoka mikoa ya pembezoni.
“Kwa sasa kuna ongezeko la mahitaji ya maziwa na uzalishaji ni mdogo na tunategemea maziwa kutoka mikoa ya Tanga na Morogoro ambako wana tusafirishia maziwa na mtindi,” alieleza.
Alisema licha ya ongezeko la mahitaji na uzalishaji kupungua, Mkoa wa Dar es Salaam hutumia aina nyingine ya maziwa yanayotoka nje ya nchi kama vile maziwa ya unga na yale yanayowe kwa kwenye vifungashio rasmi.
Kutokana na hali hiyo, kwa sasa wa zalishaji wengi wa maziwa wanakutana na changamoto za uendeshaji kutokana na kujiendesha kwa hasara kwa kuwa gharama za uzalishaiji zimebaki vilevile.
“Kwa wazalishaji wa maziwa athari wanayopitia kwa sasa ni gharama zinabaki palepale… uzalishaji unapun gua mahitaji yanaongezeka, hivyo wengi wanajiendesha kwa hasara,” alieleza.
Juma alisema kwa sasa bei ya maziwa ni Sh 2,000 hadi Sh 2,500 kwa lita, lakini kwa kipindi cha masika maziwa yanatarajiwa kupungua bei hadi Sh 1,500.
“Kwa kiangazi maziwa hufikia Shi lingi 2,000 kwa lita na maeneo mengine hadi 2,500 lakini kutokana na mahitaji kuongezeka wengi hutumia maziwa ya unga… kwa kipindi cha masika bei zinapungua kwa sababu mikoani wanapochukua huuzwa Shilingi 800 kwa lita kwa hiyo yakifika Dar es Salaam yanafika hadi Shilingi 1,500,” alisema.



