Washindi ‘Santa Mizawadi’ wajibebea pikipiki, simu

WATANZANIA kadhaa wamebadili maisha na kujikwamua kwa namna tofauti baada ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki, televisheni na simu.
Hatua hiyo ni baada ya kampuni ya mawasiliano ya simu Airtel kuhitimisha droo ya mwisho ya kampeni ya Santa Mizawadi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi, Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mbandoamesema kampeni ya hiyo ililenga kusherehekea msimu wa sikukuu kwa kuwazawadia wateja waaminifu wa mtandao huo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mbando amesema kampeni ya hiyo ililenga kusherehekea msimu wa sikukuu kwa kuwazawadia wateja waaminifu wa mtandao huo.
“Kampeni hii imekuwa sehemu ya shukrani kwa wateja wetu waliotumia huduma za Airtel, kama kutuma pesa, kujiunga na vifurushi vya Smatika, na kutumia huduma nyinginezo. Leo tunahitimisha kwa furaha kwa kuwatangaza washindi wetu wa zawadi kubwa,” amesema.
Miongoni mwa washindi wa droo hiyo ni waliotangazwa ni kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Mtwara, Shinyanga, kilimanjaro, pamoja na Mkoa wa Pwani, mlandizi. waliotumia huduma za mtandao wa Airtel kwa kutuma pesa, kujiunga na vifurushi, na kununua muda wa maongezi, walitangazwa, huku kila mmoja akieleza furaha yao kwa kupewa zawadi hizo muhimu msimu huu wa sikukuu.
Katika hotuba yake, meneja huyo amebainisha kuwa Airtel imefanikiwa kuwafikia wateja wengi kupitia kampeni hii, na itaendelea kuwawezesha kwa huduma bora na zawadi zaidi.



