Wadau waomba kuangalia upya sheria za kodi

BAADHI ya wafanyabiashara wameiomba serikali kuangalia zaidi utitiri  wa sheria za kodi  zinazowakandamiza ikiwemo ushuru wa huduma (Service Levy) unaotozwa kwenye halmashauri mbalimbali nchini ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara wanaolipa kodi serikalini

Wakitoa maoni yao mbele ya Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi inayoongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue wafanyabiashara hao jana Jijini Arusha wadau  hao mbalimbali  walisisitiza uthamini wa biashara za watanzania hata kama ni mdogo.

Wafanyabiashara hao akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Wataalam wa Kodi Tanzania Kanda ya Kaskazini, Nicholas Duhia na wengine akiwemo Adolf Locken ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji wa Abiria Moose wa Arusha(AKIBOA ) wamesema wamewasilisha maoni yao kwa tume hiyo  lakini kubwa zaidi ni kuhusu sheria za Kodi inayotozwa na Mamlakayabya Mapato Tanzania (TRA) lakini pia kodi ya huduma ishuke kutoka asilimia 3 hadi kufika 0.1 kulingana na huduma walizotoa.

“Kila halmshauri inamalipo yake katika ulipaji wa ushuru wa huduma hii ni kero lakini wamiliki wa hoteli wameongezewa kodi ya huduma ya takataka wakati magari ya kuzoa taka ni machache hivyo kodi hizi ziwekwe katika dirisha moja ili walipaji walipe kodi kwa kiwango kidogo na si kodi kubwa zaidi huku mhusika wa biashara husika hanufaiki na biashara yake”

Juliana Donald kutoka Umoja wa Wafanyabiashara Wanawake Arusha ameomba  TRA kuacha kuweka vizuizi vya kodi haswa eneo la Katesh Wilayani Hanan’g mkoani Manyara kwani linaleta usumbufu kwa kuzuia magari yenye mizigo kuendelea na safari zake badala ya kudai mhusika wa mzigo kuwa anadaiwa na mamlaka hiyo.

“TRA wanatukwaza haswa eneo la Katesh unapoagiza mzigo kutoka Singida kuja Arusha ukifika eneo hilo unazuiliwa kupita sababu unadaiwa kodi sasa mnataka tufunge viwanda vyetu au kitu gani kama tunadaiwa basi tulipe kidogo kidogo na si kuzuia gari lenye mzigo ”

Locken amesisitiza rushwa imekithiri katika ukusanyaji wa kodi ikiwemo wafanyabiashara kuulizwa maswali mengi mbele ya familia zao madukani ikiwemo maeneo ya vizuizi yanayoleta kero na kusabisha ucheleweshwaji wa mizigo huko waendako hivyo keri ni kubwa na kuomba tume hiyo kuwasaidia kurekebisha changamoto wanazokumbana nazo huko wanakofanya biashara zao.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi,Balozi Ombeni Sefue amewasihi  wafanyabiashara hao kutoa mawazo yao ili kumsaidia Rais Samia Hassan Suluhu kuja na mpango mzuri wa ukusanyaji wa kodi nchini  na kuleta nafuu kwa wafanyabiashara hao

“Hakuna mtu yoyote atakayesumbuliwa wakati wa utoaji maoni juu ya ukusanyaji wa mapato hayo lakini Tanzania bado tupo nyuma katika ukusanyaji wa mapato tupo kwenye asiliamia 12 lakini sasa tunahitaji kukusanyaji zaidi ya asilimia 15-16 ya mapato kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania “

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button