Mapigano Goma yaua watu 17

GOMA : MAPIGANO katika mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yamesababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 370.
Jeshi la Congo linaendelea kupambana na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda, ambapo hadi sasa raia wameuawa huko Gisenyi, Rwanda.
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa mzozo huu unaweza kuzua vita vikubwa vya kikanda na umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya kibinadamu huko Goma, ambapo karibu watu 500,000 wameyahama makazi yao mwezi huu pekee.
SOMA: Serikali ya DRC yathibitisha uwepo wa Rwanda Goma
Rais wa Kenya, William Ruto, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ameita mkutano wa marais wa Jumuiya hiyo kesho na kwa upande mwingine, amezitaka Ufaransa na Marekani kuunga mkono juhudi za kikanda kutafuta suluhu ya mzozo huu wa mashariki mwa Congo.



