Viongozi wa SADC kukutana kujadili vita DRC

HARARE : VIONGOZI wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wanatarajiwa kukutana leo huko Harare, Zimbabwe kwa mkutano maalum kujadili vita vinavyoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huu unafanyika huku vikosi vya kijeshi vya kikanda, vinavyoshirikiana na vikosi vya ulinzi vya Congo, vikiripotiwa kupata majeruhi baada ya waasi kuchukua sehemu ya mji wa Goma mashariki mwa DRC.

Viongozi wanatarajiwa kujadili jinsi ya kumaliza mvutano katika eneo la mashariki mwa Congo, na mustakabali wa operesheni za kijeshi za SADC katika eneo hilo. Zimbabwe, kama mwenyeji wa mkutano, imeonyesha wasiwasi kwamba mzozo huu unaweza kuathiri nchi wanachama wa SADC.

SOMA: UN yahofia kundi la waasi M23 kuingia Bukavu

Wanajeshi kutoka Afrika Kusini, Malawi, na Tanzania wameuawa katika mapigano dhidi ya waasi wa M23. Hali ya mawasiliano inazidi kuwa tete, huku Umoja wa Mataifa ukishutumu Rwanda kwa kusaidia waasi wa mashariki mwa DRC, madai ambayo Rwanda imeyakanusha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button